BETI NASI UTAJIRIKE

RASMI :KOCHA WA SIMBA AZUNGUMZIA HATMA YAKE BAADA YA KUIFUNGA RUVU SHOOTING

Kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems amefuguka hadharani kuhusiana na tetesi za yeye kuondolewa klabuni hapo. Kocha huyo alionekana kukasirishwa na taarifa  za uongo kuhusu hatma yake na amewalaumu waandishi wa habari wanaoandika habari za kupotosha na za uongo kuhusu yeye kuondoka. Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shootig kocha huyo alifanya mazungumzo na waandishi wa habari na alinukuliwa akisema 

" Tulifanikiwa kucheza mpira mzuri na niliwaomba wachezaji wangu kufunga bao la pili ili tuweze kujihakikishia ushindi na kuutawala mchezo, Tumeshinda kwa sababu ya uzoefu na nimeridhika na uwezo waliouonyesha wachezaji.

"Ninyi waandishi wa habari mnaandika vitu vya kipumbavu. Wachezaji wanapokutana na kuskia habari za mimi kuondoka wanaanza kushangazwa kwa habari wasizozijua 

" Kusema ukweli kila mwezi na kila wiki mbili napokea ofa  lakini mnaniona niko hapa na nasimamia majukumu yangu ndani ya Simba na upande wangu hakuna matatizo na hata bodi ya wakurugenzi wakitaka kuchukua hatua zozote mimi niko tayari na naheshimu maamuzi yao"

Kocha huyo alitupilia mbali masuala ya yeye kuondoka na kuendelea kuzungumzia mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

"Jambo la muhimu kwetu ni kufunga magoli na kama utakumbuka mchezo wetu na Tanzania Prisons tulipata nafasi nyingi za kufunga lakini tulishindwa.  kupata bao mapema hufungua muelekeo wa mchezo na mliona dakika 15-20 tulikuwa tukimiliki mpira na kufanikiwa kupata bao kiurahisi"

Post a Comment

0 Comments