BETI NASI UTAJIRIKE

PIGO JINGINE KWA YANGA KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA ALLIANCE FC

Klabu ya Yanga imepatwa na pigo baada ya  kuumia kwa mshambuliaji wake makini Balama Mapinduzi. Yanga wanajiandaa kukbiliana na Alliance FC ya jijini Mwanza 


 na mchezo huo wa ligi kuu Tanzania Bara unategemewa kuchezwa siku ya Ijumaa katika dimba la Nyamagana Mwanza.Balama atakuwa nje ya mchezo huo kufuatia kuumia nyonga katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya JKT Tanzania.

Taarifa zimesema kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amethibitisha kwamba Balama atakuwa nje ya kikosi sababu ya majeraha hayo

 Tayari kikosi cha wachezaji 18 kimekwisha ondoka asubuhi ya leo tayari kwa mchezo huo huku jina la Mapinduzi Balama likikosekana kwenye orodha hiyo.

Yanga ambayo ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 13 na imekwisha cheza michezo 6 itavaana na Alliance kwenye mchezo wake wa 7 na kama itashinda itafikisha pointi 16 na kupanda mpaka nafasi ya 11 na kusimama nafasi hiyo mpaka tarehe 04-Januari 2020 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya mtani wake Simba SC.

Post a Comment

0 Comments