advertise with us

ADVERTISE HERE

PELE AMTAJA MCHEZAJI BORA KATI MESSI,RONALDO NA NEYMAR

Mchezaji mkongwe wa Brazil na Santos PELE hapo jana ametoa ya moyoni kuhusu mchezaji wa Barcelona na Argentina . Pele amesema Messi ni aina ya wachezaji wanaokuja kizazi kimoja na kupotea. Mkongwe huyo mwenye rekodi ya kushinda makombe matatu ya dunia amewataja Messi ,Ronaldo na Neymar kama ni wachezaji wake bora kwa karne ya 21.
Messi mwenye miaka 32 na Ronaldo mwenye miaka 34 wameshinda tuzo mbalimbali duniani  huku Neymar akitajwa kama mchezaji ghali zaidi akitokea Barcelona kwenda PSG mwaka 2017.Pele alipoulizwa ni mchezaji yupi ungetamani kucheza naye alinukuliwa " Nafikiri Messi kwanza anatoa pasi nzuri za kufunga, anapiga chenga anauwezo wa kukaa na mpira, Kama tungekuwa timu moja basi wapinzani walitakiwa waogope wachezaji wawili na si mmoja . Kwa sasa Messi ni mchezaji aliyekamilika "

Mkongwe huyo aliendelea kusisitia kuwa wachezaji wazuri walikuwa wengi enzi hizo

" kipindi chetu kulikuwa na wachezaji wengi nyota akiwemo Maradona ,Garincha, Eusebio,Didi ,Cruffy ila kwa sasa tunao wawili kama si watatu. Tuna messi ,Ronaldo na kidogo Neymar ila bado hajaonyesha ubora wake kwa timu ya taifa Brazil.

Ningependa kuona Neymar anashinda kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar ili waweze kurudisha heshima kwa bara la kusini heshima iliyopotea kwa miongo miwili. Watu wanamzungumzia Neymar kwa mabaya na mimi pia nilishawahi kumzungumzia ila tunasahau ni zao letu la Santos, nyakati nyingi nimekuwa nikizungumza na baba yake kuhusu yeye na ni mchezaji mzuri"

Post a Comment

0 Comments