BETI NASI UTAJIRIKE

PATRICK AUSSEMS : NINARUDI BAADA YA SIKU MBILI NA SINA MPANGO WA KUONDOKA SIMBA

Kocha mkuu wa timu ya Simba SC amezima tetesi zilizoenea kwamba ameondoka klabuni hapo na kurudi kwao Ubelgiji. Aussems ametumia mtandao wake wa twitter kuelezea


uwepo wake ndani ya Simba na atarejea nchini tarehe 21 Novemba. Hapo jana taarifa zisizo rasmi zilisambazwa na vyombo mbalimbali vya habari vikisema Aussems ameachana na timu ya Simba, baada ya uchunguzi wa amospoti.com iligundulika ni kweli Aussems ameondoka nchini na sababu kubwa ilikuwa ni matatizo ya kifamilia na atarejea siku chache zijazo.

Baada ya tetesi hizo kusambaa kila kona ilimlazimu Aussems kuandika tweet na kutoa taarifa sahihi ya safari yake na hii ni tweet yake.

Kocha huyo aliandika "Nililazimika kuondoka kwa siku mbili kwa sababu zangu binafsi.Nitarudi kesho kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting na tutapata pointi tatu"

wachezaji wa Simba wanaendelea na mazoezi makali kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa tarehe 24 Novemba na kocha Aussems ataongoza kikosi hicho.








Post a Comment

0 Comments