BETI NASI UTAJIRIKE

NYOTA WENGINE WATATU YANGA KUIKOSA ALLIANCE FC LEO,SABABU ZATAJWA

Viungo watatu wa Yanga Abdulaziz Makame, Feisal Salum n Mohammed Isaa "Banka" wataukosa mchezo wa ligi kuu Tanzania dhidi ya Alliance utakaopigwa leo jijini Mwanza kwenye uwanja wa Nyamaga. Wachezaji hao wako kwenye kambi ya timu ya taifa ya Zanzibar ambayo imeana maandalizi ya michuano ya CECAFA Challenge inayoanza Disemba 7 nchini Uganda.

Uongozi wa Yanga umesema baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania wachezaji hao walipewa ruhusa kwenda kujiunga na kambi ya Zanzibar Heroes

Hata hivyo baadae bodi ya ligi iliwataarifu kuwa wanapaswa kucheza michezo miwili ya viporo dhidi ya Alliance na KMC mchezo utakaopigwa disemba 02 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Kaimu kocha mkuu wa klau hiyo Bw.Charles Mkwasa mesema pamoja na kuwakosa nyota hao bado aa matumaini ya kufanya vyema kwenye michezo hiyo.

Baadhi ya mashabiki wamekerwa na uongozi wa Yanga kuruhusu wachezaji hao kuondoka ilihali wana michezo miwili muhimu. Kama Yanga atashinda mechi zote za viporo atajikusanyia pointi 25 na kukaa kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara.

Post a Comment

0 Comments