BETI NASI UTAJIRIKE

NEYMAR NA POGBA WAPIGWA CHINI TUZO HIZI

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013  Mchezaji Paul Pogba na Neymar JR wamekosekana kwenye kikosi cha wachezaji 50 bora wa duniani.


Tuzo hizo hutolewa na mtandao wa GOAL 50 na Neymar amekuwa ni mmoja wa wachezaji 50 tangu mwaka 2011 huku akishika nafasi ya 4 mwaka 2015 baada ya kuisaidia Barcelona kutwaa makombe 3.

Misimu miwili iliyofuata mchezaji huyo alikuwa ndani ya 10 bora lakini majeraha  yalimponza na katupwa nafasi ya 24 msimu uliofuata. Neymar amekosekana kwenye tuzo hizo baada ya kucheza michezo michache huku timu yake ya taifa Brazil ikishinda Copa America bila ya uwepo wake.

Kwa upande wa Pogba mchezaji huyo ni tofauti kwani alikuwa na wakati mgumu alipocheza chini ya Mourinho na hakuweza kuonyesha uwezo wake mpaka Ole Gunnr alipoichukua Manchester United ambapo alionyesha kiwango kizuri lakini baadaye alishuka kiwango chake.

Moja ya mambo yanayotajwa kuharibu uwezo wa mchezaji huyo ni kauli yake kwamba anataka kuondoka klabuni hapo ili akakutane na changamoto mpya. Awali mchezaji huyo alitajwa kuhamia Real Madrid. Taarifa zinasema Pogba alishaanza kutokuwa makini na mazoezi ya Ole Gunnar akiamini ataondoka msimu uliopita

Post a Comment

0 Comments