advertise with us

ADVERTISE HERE

MZUNGU WA TAIFA STARS AZUA BALAA UWANJA WA TAIFA

Mzungu anayefahamika kwa jina la Bongo zozo ameendelea kuwa gumzo kwa mashabiki wa soka la Tanzania baada ya siku chache zilizopita kununua tiketi 100 maalumu kwa wanawake akiwataka wajitokeze uwanja wa taifa kuishabikia timu hiyo.


Bongo zozo hakuwa nyuma siku ya jana kuisapoti Taifa Stars kwani aliwasili uwanjani hapo saa 1:26 na kuibua shangwe kwa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo.

Bongo zozo aliwasili uwanjani hapo na marafiki zake wawili na baada tu ya kuingia mashabiki walianza kumshangilia huku yeye mwenyewe akihamasisha shangwe hizo zilizowatisha Equatorial Guinea 

Bongo zozo ni shabiki mkubwa wa Taifa Stars na aliwahi kusafiri mpaka nchini Miri kutazama mechi za timu hiyo iliposhiriki AFCON kwa mara ya kwana baada ya miaka 39. Mbali na hayo pia Bongo zozo amekuwa akijichora bendera ya taifa la Tanzania na anaongea kiswahili sahihi.

Post a Comment

0 Comments