MWAKALEBELA ALUSHA DONGO KWA SIMBA

Makamu mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema klabu hiyo ipo kwenye michakato ambayo wamejiwekea kama klabu na sio kwamba wamefanya hivyo baada ya



 kuona watani zao Simba wamekamilisha ujenzi wa uwanja wa mazoezi Bunju.Aidha mwakalebela amesema hata utaratibu wa kukamilisha miradi mingine iko tofauti . Uwanja wa Yanga unajengwa na wanayanga wenyewe huku wa Simba umejengwa na Mo 

Mwakalebela amenukuliwa akisema "Sisi hatushindani na Simba katika ujenzi wa uwanja wetu. Tunatekeleza mipango ambayo tumejiwekea. Hata vipaumbele ni tofauti ,Simba wamejengewa uwanja na Mohammed Dewji wakati klabu ya Yanga itajenga uwanja wake kwa nguvu za wanaYanga wenyewe"

Yanga imeshaanza mchakato wa kujenga viwanja vyake vitatu eneo la kigamboni walilopewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda.

Wakati huo Yanga inaendelea na ukarabati wa uwanja wake wa Kaunda . hata hihivyo ukrabati wa Kaunda kwa sasa umesimama kupisha mradi wa serikali wa kudhibiti mafuriko eneo la Jangwani .

Mh.Makonda amesema mradi huo ukikamilika suala la mafuriiko litabaki historia eneo hilo la Jangwani

Post a Comment

0 Comments