advertise with us

ADVERTISE HERE

MSEMAJI WA YANGA ANTONIO NUGAZ ALIA KLABU HIYO KUPIGWA NA WAJANJA WA MJINI

Afisa Muhamasishaji Mkuu wa Yanga Antonio Nugaz amewataka wanaouza na kununua jezi feki za Klabu hiyo kuacha kufanya hivyo kwani ni sawa na kuihujumu Klabu hiyo.Nugaz amenukuliwa akisema :


"Sisi kama Young Africans sports club baada ya kupigiwa simu kwamba operesheni kupiti GSM itafanyika kwahiyo mimi nikasema okay ngoja niigie kwa sababu ya timu ya wananchi, zile milioni 10 ,20 pesa za usajili na vitu kadha wa kadha zinatoka kwenye mauzo ya jezi. Sasa kama mtu hauzi jezi orijino inamaana haitakii mema young Africans inamaana huyo ni muhujumu Yanga. Brand chapa GSM wao ndio wana mamlaka ya kuuza, kuchapisha na kutoa jezi zote kwa ajili ya msimu wa 2019/20 hii ni official kit supplier kwa kushinda tenda. Kwa aliyefanya hivi na anayefanya hivi ujue kabia wewe shabiki wa Yanga ambae hununui orijino unaihujumu timu yako. Mnalalamika Dante halipwi kumbe hela wanachukua wajanja wajanja mjini hapa"  
Ametoa kauli hiyo wakati Viongozi wa Klabu ya Yanga wakiongozwa Na Mdhamini wao GSM walipofika Mtaa wa Agrey na Congo Kariakoo, DSM na kukamata jezi feki.

Post a Comment

0 Comments