Kocha mteule wa muda mfupi wa klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwasa ameanza kuwanyoosha wachezaji wake mara baada ya kukabidhiwa timu hiyo.
"Mpo hapa kuipigania klabu hii na kubeba vikombe, hilo ndo lengo la kwanza kwa kila mchezaji anayeitumikia klabu hii . tunapaswa kuishi katika utamaduni huu na ili kutimiza dhamira hii ni lazima tuanze kushinda michezo yetu . tutakaposhinda kila kitu kitarejea katika hali yake,uwanja utajaa na furaha kwa mashabiki itarejea.. Nyie ni wachezaji wazuri sana nami nipo hapa kuwasaidia kufanikisha yote hayo"
Yanga ipo mkoani Mtwara kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC mchezo utakaochezwa uwanja wa Nangwanda jioni ya leo. Matarajio ya wanayanga ni kuona timu hiyo inashinda na kurejea kwenye nafasi za kugombea ubingwa wa ligi kuu.
0 Comments