Kiungo wa Taifa Stars na klabu ya Simba ameonekana kukerwa na habari za uongo zilizoeneza dhidi yake kuondoka kambi ya taifa stars kwa madai ya kuidai timu hiyo fedha
Mwandishi mmoja wa kituo cha EATV afahamikae kama Abdul aliandika habari hizo za uzushi na mkude alionekana kukerwa na habari hizo kwani hazina ukweli wowote na yeye aliondoka kambini Tiafa Stars kwa sababu za kifamilia.
Mwandishi huyo aliandika hivi " Viongozi wa mpira wa nchi hii hawapendi kuambiwa ukweli Jonas Mkude hana matatizo ya kifamilia wala nini mlipeni posho zake zote ndo alipoti kmbini mbona mnakuwa washwahili kiasi hiki ... Mliwahi kutka kuwadhulumu wakidai mnasema hawana nidhamu... kama kuna mwandishi atawza kuja kufanya habari za kchunguzi TFF kuna madudu sana....
Kiongozi wa juu huwezi kuwa na power ya kuwaambia wachezaji hawatocheza national timu wewe kama nani? mmepiga stop Manula kwa husda za kijinga , mmemfukuza Ammy kwa husda za kijinga"
Jonas mkude aliscreenshot ujumbe huo na kuandika hivi
"Kwa kipindi cha hivi karibuni, ndugu zangu Waandishi wa habari wamekuwa wakifanya jitihada kubwa katika kujenga uzalendo na hamasa kwa timu yetu ya Taifa,
lakini kwa masikitiko makubwa nimeshtushwa na habari ya huyu mwandishi Abdulaziz Mrisho wa kituo cha East Africa Radio/TV.
Hiki alichokiandika si cha kweli na kina mlengo wa kuharibu umoja wetu kama Watanzania kuelekea mchezo wetu wa Ijumaa, lakini pia kunitengenezea chuki kwa Watanzania na Shirikisho.
Pamoja na hilo, nimepanga kuchukua hatua za kisheria kwa muhusika na niwaombe Watanzania wapuuzie uzushi huo na tuelekeze nguvu zetu katika mchezo wetu dhidi ya Equatorial Guinea. Asanteni"
0 Comments