ads

adds

MKUDE AONDOKA KAMBI YA TAIFA STARS, SABABU ZATAJWA

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa rasmi ya mchezaji wa klabu ya Simba na Taifa Stars kuondoka kwenye kambi ya mazoezi inayojiandaa na michezo miwili



 ya kimataifa kati ya Equatorial Guinea na Libya itakayofanyika siku ya ijumaa uwanja wa taifa .jijini Dar es salaam na ule wa pili dhidi ya Libya utafanyika nchini Tunisia.


Kocha Mkuu wa Taifa Stars Ettiene Ndairagije amempa ruhusa Kiungo Jonas Mkude kuondoka kwenye Kambi ya Kikosi hicho kwenda kushughulikia masuala yake ya kifamilia.
Mkude alitoa taarifa kwa Kocha Ndairagije kuomba ruhusa ya kutojiunga Kambini ili kushughulikia masuala ya kifamilia,ruhusa ambayo alipewa kabla ya kuanza kwa Kambi Jumamosi.
Jana Jumatatu Mkude aliripoti Kambini na kumueleza Kocha Ndairagije kuwa bado hajamaliza masuala anayoshughulikia hivyo Kocha amempa ruhusa nyingine ya kumaliza jambo hilo linalomkabili.
Kulingana na muda mfupi uliobaki kuelekea mchezo dhidi ya Equatorial Guinea Kocha Ndairagije hataweza kuongeza mchezaji mwingine.


Post a Comment

0 Comments