BETI NASI UTAJIRIKE

MKONGO MWINGINE KUTUA YANGA MWISHONI MWA MSIMU

Klabu ya Yanga ilitangaza uwepo wa kocha anayekaimu nafasi ya Zahera kuendelea mpaka mwishoni mwa msimu wa 2019/20. Mkwasa ameendelea kufanya vizuri tangu alipokabidhiwa timu hiyo na kufanikia kushinda michezo miwili ya ligi 

Mbali na uwepo wa mkwasa lakini klabu hiyo imeonekana kuhitaji kocha wa kudumu klabuni hapo.inaelezwa  Kocha wa As Vital ya DR Congo, Frolent Ibenge, ameingia kwenye rada za kuchukua nafasi ya Zahera.

Kocha ameanza kuhusishwa na tetesi hizo kufuatia kufanya vizuri akiwa na Vital ambayo inashiriki Ligi Kuu Congo.

Ibenge ambaye ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Congo, amekuwa akifanya na Zahera kama Msaidizi wake katika kikosi cha taifa hilo.

Licha ya taarifa hizi kuenea, uongozi wa Yanga umeshindwa kuzizungumzia na badala yake umesisitiza kuwa mpaka muda mwafaka ufikie wataweza kuzungumzia mbadala wa Zahera,

Ikumbukwe Frolent Ibenge na Mwinyi zahera ni makocha wakuu wa timu ya taifa Congo na waliisaidia timu hiyo kufika hatua ya mtoano michuano ya AFCON

Post a Comment

0 Comments