advertise with us

ADVERTISE HERE

MIRAJI ATHUMANI ANAVYOZIDI UKARIBIA UFALME PALE SIMBA

Wiki chache niliwahi kuandika jinsi Miraji Athmani anavyounyemelea ufalme kwenye klabu ya Simba na sasa naona ufalme umeanza kumfuata yeye. Nyota huyo ameanza kuabudiwa 


na viongozi kwa  amepewa ulinzi maalumu ndani ya Simba ambao utamwezesha kuwa katika afya nzuri muda wote.Hatua hiyo, imekuja baada ya mchezaji huyo hivi karibuni kukosekana katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ambayo Simba ilishindwa kupata ushindi baada ya kusumbuliwa na maumivu ya mwili.

Mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Simba ambaye ameomba hifadhi ya jina lake, alisema kuwa hivi sasa Sheva pamoja na wachezaji wengine, wamepewa ulinzi maalumu. 


Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha mechi ya timu ya taifa.

“Lakini jambo kubwa ambalo kwa sasa lipo kikosini kwetu ni mkakati kabambe kuhusiana na wachezaji, kwani hivi sasa wamepewa ulinzi mkubwa wa afya zao. Madaktari wametakiwa kufanya kazi yao ipasavyo ili kila mchezaji awe fiti muda wote


Kukosekana kwa Miraji  katika mechi yetu na Prisons lilikuwa ni pigo kwani pengine angekuwepo tungepata ushindi kutokana na aina ya uchezaji wake,” alisema kiongozi huyo.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alisema: 


Afya za wachezaji ni jambo muhimu sana kwangu, kwani unapokuwa na majeruhi wengi timu itakumbana na changamoto nyingi uwanjani kwa hiyo ni lazima tuwe makini kuhakikisha wanakuwa fiti muda wote."

Post a Comment

0 Comments