BETI NASI UTAJIRIKE

MIRAJI ATHUMANI AMTANGAZIA VITA MEDDIE KAGERE

Miraji Athuman ‘Madenge’, ameingia kwenye vita ya kuwania kiatu cha ufungaji bora kwa kutamka naye anakitamani kiatu hicho.Madenge ameyatamka hayo ikiwa ni baada ya 


kufikisha mabao sita akiwa nyuma ya kinara anayeongoza katika chati hiyo, Meddie Kagere kwa mabao mawili tu. Kagere ana mabao 8 .Sheva ambaye alianzia katika kikosi cha vijana cha Simba, ameiambia amospoti.com kuwa kiatu hicho cha ufungaji bora atakitwaa endapo atapangwa mshambuliaji wa kati kama ambapo anatumika kwa sasa.

Unajua mimi ni winga lakini kwa siku hizi mwalimu amenibadilishia nafasi na nimekuwa nikitumika kama mshambuliaji wa kati na siyo kutokea pembeni tena.

“Kama nikiendelea kucheza eneo hili, nina uhakika kuwa naweza kuibuka na ufungaji bora kwa sababu najituma na kupambana katika kila mechi nifunge na unaona juhudi zangu zinazaa matunda.

“Kitu kikubwa mimi napambana tu pale ambapo ninapewa nafasi na hiyo ndiyo imekuwa siri kubwa sana ya kuwa na kiwango ambacho ninacho kwa sasa,” alimaliza Sheva.

Post a Comment

0 Comments