BETI NASI UTAJIRIKE

MIRAJI ATHMANI AJA NA STAILI MPYA SIMBA

Mshambuliaji kinda na hatari wa klabu ya Simba Miraji Athmani amelazimika kunyoa nywele zake alizokuwa amezisokota tangu mwanzoni mwa msimu wa 2019/20


Kwa sasa ukimuona Madenge unaweza usimfahamu kirahisi kutokana na kubadilisha muonekano wa kichwa chake.

kwenye mazoezi ya Simba yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Gymkhana, ameonekana na staili mpya ya nywele.

Inaelezwa kuwa, Sheva ameamua kunyoa nywele hizo, kutokana na ushauri aliopewa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo, wakidai kuwa mtindo wa awali ni wakihuni na hauendani na umri wake.

amospoti.com, lilipata nafasi ya kuzungumza na Sheva, ambaye alisema kuwa: “Nimeamua kunyoa hivi ili niwe na muonekano tofauti, hakuna jambo lingine.”

Post a Comment

0 Comments