advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA WASHINDWE WAO TU ILA MGHANA YUPO TAYARI KUTUA

Mchezaji wa klabu ya Rayons Sports ya Rwanda ameanza kuwahakikishia mashabiki wa Yanga uwezekano wa yeye kutua klabuni hapo hivi karibuni . 

Raiahuyo wa Ghana amekuwa ni nguzo muhimu kwenye klabu yake ya Rayon Sports kwa kufunga mabao 2 kwenye mechi 8 na kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 15 nyuma ya vinara Police FC na APR zenye pointi 18 kila moja.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ,Mchezaji huyo alionekana kuwashukuru mashabiki wa Rayon Sports na aliandika


 " Mungu mwenyewe anajua jinsi gani ninavyowafanya watu wajiskie . Siku zangu ndani ya Rayon sports zilikuwa nzuri sana. Asante Rayons kwa kujitokeza kwenu na kuonyesha upendo wa kweli"

Bado haijawa rasmi kama mchezaji huyo ataendelea kuwepo Rayon ama ujumbe huo ni kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo na kutua Yanga 

Endelea kuwa karibu na amospoti.com kwa taarifa za kimichezo.

Post a Comment

0 Comments