advertise with us

ADVERTISE HERE

MFALME MPYA WA REAL MADRID ,RONALDO TUPA KULE

Mashabiki wa klabu ya Real Madrid maarufu kama " Madridista" wameshaanza kurusha maneno kwa mshambuliaji hatari zaidi aliyewahi kuitumikia klabu hiyo na kuipa mafanikio


 makubwa Cristiano Ronaldo na jeuri hiyo imeanza baada ya kinda wa klabu hiyo kufunga mabao 3 kwenye mchezo wa  ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya galatasary.

Mchezo huo ulimalizika kwa Real Madrid kushinda mabao 6-0 huku rodrygo akifunga mabao akika ya 4,7 na 90+2 ,Karim Benzema amefunga mabao 2 dakika ya 45 na 81 na Sergio Ramos akifung bao moja kwa mkwaju wa penati dakika ya 14.

RODRYGO NI NANI?

Rodrygo Silva  de Goes ni kinda wamiaka 18 mwenye asili ya brazil anayeitumikia klabu ya Real Madrid kama mshambuliaji. 

Rodrygo alizaliwa tarehe 9 January 2001 nchini Brazili na alijiunga na timu ya vijana ya Santos mwaka 2011 akiwa na miaka 10 tu. Mwaka 2017 alisaini mkataba wake wa kwanza kuichezea Santos na alifanikiwa kucheza michezo 41 akifunga mabao 9 kutoka mwaka 2017-2019.

Mwaka 2019 alifanikiwa kusainiwa na Real Madrid timu ya vijana akicheza michezo 2 na kufunga bao 1. Klabu hiyo iliuona uwezo wake na kumpandisha timu ya wakubwa . Amecheza michezo 5 na kufunga mabao 5 ikiwemo Hat trick dhidi ya Galatasary.

Rekodi timu ya taifa Brazil

Rodrygo ameichezea brzil U17 mechi 4 na kufunga mabao 3, Brazil mechi 10 kifunga mabao 3 na Brazil U23  akiwa bado hajafunga.

Mashabiki wamzodoa Ronaldo 

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo ameendelea kukalia kuti kavu baada ya kucheza michezo 4 ya UEFA akifunga bao 1 tu. Mshambuliaji huyo amekuwa na wakati mgumu klabuni hapo kwani hata mashabiki wa juventus wamekuwa hawafurahishwi na mwenendo wake. 

Kwa upande wa Mashabiki wa Real Madrid walianza kumtaja Rodrygo kama nyota hatari zaidi wa klabu hiyo na hakuna kama yeye.


Post a Comment

0 Comments