BETI NASI UTAJIRIKE

MESSI AANZA KUTANGAZA BALAA JINGINE KUELEKEA BALLON 'D OR

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi ameonekana kutamani kutwaa tena tuzo ya Mchezaji bora wa dunia kwa mara 6. Messi mwenye umri wa miaka 32 amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo mara 5 kutoka mwaka 2009,2010,2011,2012 na 2015 sawa na mpinzani wake Cristiano Ronaldo aliyetwaa tuzo hiyo mwaka 2008,2013,2014,2016 na 2017 huku Luka Modric akiitetea tuzo hiyo kwa kushinda mwaka 2018.

Hivi karibuni mchezaji huyo alifanya mahojiano na vyombo vya habari na kuzungumzia tamaa yake kutwaa tena tuzo hizo messi alinukuliwa akisema 

"Ni jambo la heshima na kipekee kushinda tuzo za Ballon D'or ,Kushinda tuzo hizi si juhudi binafsi bali ushirikiano wa timu nzima.

"Nakumbuka mwaka 2010 wachezaji watatu kutoka timu yetu waliichaguliwa kuwania tuzo hizo nikiwemo mimi,Iniesta na Xavi, Uwepo wetu ndani ya klabu yetu na ushirikiano vilileta matokeo chanya kwenye yetu klabu na heshima kati yetu. Binafsi naziheshimu n kupenda kutwaa tena tuzo ya Ballon d'Or"

Messi ni mmoja ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hizo kwa mwaka 2019 na mshindi atatangazwa mwezi Disemba.

Post a Comment

0 Comments