BETI NASI UTAJIRIKE

MBWANA SAMATTA AFUNGA ILA UEFA NDIYO BASI TENA

Mshambuliaji hatari wa KRC Genk Mtanzania Mbwana Ally Samatta ameshindwa kuisaidia timu yake kufuzu hatua ya mtoano ligi ya mabingwa ulaya baada ya timu hiyo kuambulia 


pointi 1 tu kwenye michezo mitano iliyocheza kwenye kundi E. Hapo jana usiku Samatta alifaniiwa kufunga bwao dakika ya 85 ingawa waliambulia kipigo cha nne dhidi ya Red Bull Sarlzburg kwa kufungwa mabao 4-1 wakiwa uwanja wa nyumbani ubelgiji.

Genk walipata sare 1 tu dhidi ya Napoli na kuwafanya wabuluze mkia kundini humo kwa kufungwa mabao 16 na wao kufunga mabao 5 tu huku mawili yakifungwa na Mbwana Samatta.  Kundi hili linaongozwa na Liverpool wenye pointi 10 wakifuatiwa na Napoli wenye pointi 9 na nafasi ya tatu ni Red Bull Sarlzburg. 

Kupata pointi moja kwa KRC Genk kunaifanya klabu hiyo kuingia moja kwa moja kwenye hatua ya mtoano kombe la UEFA EUROPA LEAGUE lenye washiriki kama Arsenal na Manchester United.

Post a Comment

0 Comments