ads

adds

MASHABIKI WAGOMA KUMSAMEHE KOCHA MGUNDA BAADA YA USHINDI DHIDI YA EQUATORIAL GUINEA

Kocha msaidizi wa timu ya "Taifa Taifa Stars " ameendelea kukalia kuti kavu mbali na kwamba timu hiyo imeshinda mchezo wake dhidi ya Equatorial Guinea



Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa na kuishuhudia Taifa Stars ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 . Mabao ya stars yalifungwa na Msuva dakika ya 68 na Abubakar Salum "SURE BOY' dakika ya 90 na kuifanya timu hiyo kuongoza kundi lao lenye timu za Tunisia,Libya na Equatorial Guinea.


Mashabiki wameendelea kulalama na kuhoji kwanini amemuacha kipa bora zaidi Tanzania Aishi Manula  na kulaani vikali goli alilofungwa kaseja kwamba ni jepesi na mno.

Bifu lipo hivi kati ya Mgunda na mashabiki wa Stars : 

Wakati wachezaji wa timu ya Taifa wanaitwa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Equatorial Guinea jina la mlinda mlango wa Simba Aishi Manula halikuwemo hivyo mashabiki walihoji kwanini jina hilo halimo ndipo kocha msaidizi wa Taifa Stars akanukuliwa akisema 

"Hatumchagui mtu kwa sura yake kwa sababu hatukuja kuposa sisi, Tunachagua mchezaji Mtanzania mwenye uwezo wa kucheza" .

Mashabiki walimjia juu na kumlazimisha abadili kauli yake kwa kusema 

WaTanzania wameninukuu vibaya. Mimi nilitoa kauli ile kwa nia nzuri tu nimeshtuka sana kwani imesambazwa sana wakati mimi nilikuwa na nia nzuri tu.Manula ni Mchezaji wa Tanzania na amefanya makubwa ninacho waomba wa-Tanzania wawe kitu kimoja waje waishangilie Timu yao ya Taifa" 

Baada ya kukiri kosa mashabiki walikaa kimya wakiusubiri mchezo wa Stars na Guinea. Guinea walipopata bao la kuongoza dakika ya 17 kila shabiki alianza kumlaumu kocha mgunda kwa aina ya goli jepesi alilofungwa Kaseja .

Bado kocha huyo anachangamoto ya kujieleza kwanini alimuacha kipa aliyefungwa mabao 3 tu ligi kuu Tanzania Bara kwenye mechi 8 alizocheza. Swali ni je kwanini Mgunda hakumuita  Manula kwa sababu zipi 

Post a Comment

0 Comments