advertise with us

ADVERTISE HERE

MANENO YA KOCHA WA SIMBA KUELEKEA MCHEZO NA RUVU SHOOTING "WAPAPASAJI"

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameendelea kujinoa kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ddhidi ya Ruvu Shooting. Kocha huyo amefurahishwa kuona ushindani 


uliopo katika ligi hiyo msimu huu  na kueleza kuwa hali hiyo inaongeza umakini kwenye timu yake.

Aussems alisema ushindani pia unasaidia kuimarisha viwango vya wachezaji kwa sababu kila mmoja anajiimarisha ili apate namba katika kikosi cha kwanza.

Aussems alisema ushindani unapokuwa mkubwa, kila timu inalazimika kuongeza mbinu za kusaka ushindi kwa sababu hakuna anayeamini atapata matokeo mazuri kabla ya kuingia uwanjani.

"Ushindani ni mzuri, utafanya kila mmoja afahamu hayuko mahali salama, hakuna jambo jepesi, tunajiimarisha kila siku, kwa sababu tunataka kupata matokeo mazuri, hakuna mechi nyepesi,hakuna mwenye uhakika wa kushinda nyumbani au ugenini," .

Mbelgiji huyo aliongeza kuwa mbali na ushindani katika ligi, pia katika kila timu kuna ushindani hali hii inasaidia kuwafanya wachezaji "waamke" na kujipanga kupambana.

"Mechi ni ngumu, timu zimeimarika, kila upande sasa unafanya vizuri, tayari wachezaji wameimarika tofauti na tulivyoanza msimu, ili tufikie malengo, tunatakiwa kujituma zaidi," alimaliza  kocha huyo.

Alisema kuwa baada ya kuwapa mapumziko wa siku mbili, kikosi chake kilianza mazoezi ya
kujiandaa na mechi dhidi ya Ruvu Shooting, na anaamini ataendelea kuwatumia wachezaji wote waliosajiliwa kulingana na aina ya mpinzani wanayekutana naye.

Post a Comment

0 Comments