advertise with us

ADVERTISE HERE

MANENO YA KOCHA WA SIMBA BAADA YA SARE NA PRISONS TANZANIA

Klabu za Simba na Prison Tanzania zimetoka suluhu ya kuofungana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Mchezo uliopigwa dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam. 


Mchezo huo umeibua hisia zaidi kwa mashabiki wa Simba wakilaumu kikosi cha Mwalimu Aussems kwa kuwaacha baadhi ya wachezaji kama Athmani Miraji  na wengi wameilaumu timu hiyo kwa kutoweka kambi tangu imerudi toka Singida.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Aussems alisema 

" Tangu nimekuja Tanzania sijawahi kuona timu iliyojipanga dimbani kama hii kwa sasa sishangai kuona kuwa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hadi sasa, walicheza kwa  kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza"

Kwa matokeo ya mchezo huo Simba inaendelea kuongoza ligi ikicheza michezo 9 na kushinda michezo 7 sare 1 na kufungwa 1 hivyo kujikusanyia pointi 22 nafasi ya pili ni Lipuli Fc wakicheza michezo 10 na kujikusanyia pointi 18 ,Kagera Sugar ni nafasi ya tatu akiwa na pointi 17.

Post a Comment

0 Comments