advertise with us

ADVERTISE HERE

MANARA : SAMATTA NI BABA LAO ANASTAHILI HESHIMA YA KIPEKEE

Msemaji wa Klabu ya Simba  na mjumbe wa kamati ya ushindi Taifa Stars Haji Manara amefurahishwa na kiwango cha Mbwana Samatta anachokionyesha Ulaya 


hasa baada ya kufunga bao la kichwa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Liverpool..

Samatta ameingia kwenye vitabu vya kihistoria kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania aliyefunga bao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool kwenye dimba la Anfield. Kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON kati ya Taifa Stars na Equetorial Guinea na Libya Manara alifanya mkutano na waandishi wa habari kumwombea heshima mbwana samatta kwa watanzania na alinukuliwa akisema 

"Kuhusu Mbwana ,Leo asubuhi nilitumiwa meseji na mtu mmoja anaitwa mkubwa kambi ni maarufu sana mitandaoni . Anasema hivi hatuwezi kutoa tuzo yoyote ya heshima maana kibadeni alipewa uchifu wa wangoni akaitwa  Chief Mputa  . Hatuwezi kutoa tuzo sisi kama wazaramo  na kumpa uchifu pale mbagala maana amefanya mambo makubwa , Kufunga ndani ya Anfield sio utani, Binafsi simjui muafrika mashariki aliyewahi kufunga pale na sio goli la kawaida ni Bombastic header . 

Yaani mtu karuka alafu mbele ya mabeki wakubwa akiwemo Kapteni Milner alafu unafunga anfield , maana wanasema ule ni uwanja ambao mpinzani anaanza kufungwa kabla ya mchezo maana shangwe za mashabiki ni kubwa  hasa unapopigwa ule wimbo wa this is Si... Anfield. Kufunga bao kwa samatta si vitu vya kawaida , hiyo ni rekodi ambayo watanzania lazima tujivunie . Sisi kama watanzania tuonyeshe shukrani yetu kwa kujaa uwanjani kumwonyesha kapteni wa Nchi asante, Pale Tanzania nzima imetangazwa . Mtangazaji anasema msimu uliopita amefunga mabao 32 na anamtaja ni Kapteni wa Tanzania. Zamani likuwa ni ndoto tulikuwa tunaona akina Robi Folla,Eto'o na Kanu ila sasa hivi anafunga mtanzania ndani ya anfield. Kule VAR iliharibu mchezo ila tunahesabu lile limo . Tuandike alichokifanya Samatta na tuutangazie ulimwengu"

Post a Comment

0 Comments