Wakati Simba ikijiandaa kuhamia Bunju hali ni tofauti kwa klabu ya Yanga kwani mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amewaomba wawe na subira kuhamia Kigamboni
Yanga wameambiwa waendelee kubakia Jangwani baada ya kukabidhiwa eneo ambalo watalitumia kujenga uwanja wake wa mazoezi huko Kigambon,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka Yanga kutokuwa na haraka ya kuhamishia makazi hayo katika eneo hilo na badala yake akiwataka waendelee kuwa na subira.
Makonda ameeleza kuwa kwa sasa serikali ina mikakati kabambe ya kuhakikisha eneo la Jangwani linawekwa sawa kwanza kutokana na changamoto kadhaa zilizopo.
Muonekano wa kiwanja cha Yanga Kaunda wakati wa mvua huwa na muonekano huo na kipo pembeni ya ofisi kuu za klabu hiyo.
Ameeleza kwa kuwataka wanayanga wote wawe na subira kutokana na kiu waliyonayo lakini ahiahidi mambo yataenda vizuri kwa ajili ya kukarabati eneo hilo.
"Ndugu zangu wa Yanga msiwe na haraka.Msihame Jangwani kwa sasa. Serikali makini ya Rais John Magufuli italifanyia kazi eneo la Jangwani ambalo limekuwa na changamoto kwa muda mrefu na hivyo kila kitu kitaenda sawa."
0 Comments