Klabu ya Barcelona ilipoteza mchezo huo kwa kupigwa mabao 3-1 dhidi ya Levante. Barcelona walianza kupata bao kupitia Lionel Messi dakika ya 38 huku Levante wakichmoa na kuongeza kuanzia dakika ya 61,63 na 68 .Klabu ya Barcelona ilianza vibaya msimu huu lakini baadaye ilirejea nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi ikicheza michezo 11 kushinda 7 sare 1 na kufungwa 3 ikijikusanyia pointi 22 na kuongoza ligi.
Upande wa wapinzani wake Real Madrid na Atletico zimekuwa ni timu ambazo hazielewi zinataka nini msimu huu. Real Madrid ilijikuta ikipata sare ya 0-0 kutoka kwa Real Betis. Madrid walijaza nyota wake wote akiwamo mchezaji bora wa dunia tuzo za Ballon d'or Lukas Modric , Kroos, Benzema ,Hazard lakikni hawakuambulia kitu. Kama Real Madrd angeshinda mchezo huo angekaa kileleni mwa ligi akiwa na pointi 24 ila kwa sare hiyo ameendelea kushika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi akizidiwa magoli n Barcelona inayoongoza ligi.
Atletico Madrid na yeye aliambulia sare ya mabao 1-1 na kumfanya abakie nafasi ya 3 akiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 12 na kushinda mechi 5 Sare 6 na kufungwa 1.
Upande wa mfungaji bora bado nyota wa Villa Real anaongoza orodha hiyo akiwa na magoli 8 akifuatiwa na Benzema mwenye magoli 7
0 Comments