BETI NASI UTAJIRIKE

LIONEL MESSI AWEKA REKODI MPYA BARCELONA

Mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2019 Lionel Messi ameweka rekodi mpya kwenye maisha yake ya soka baada ya kufikisha mchezo wake wa 700 tangu kuanza kucheza soka 


la kulipwa kwa ngazi ya klabu.Messi amezitumikia timu mbili tu kwenye maisha yake ya soka la kulipwa nazo ni Barcelona na timu ya taifa Argentina alyoichezea michezo 138. Nyota huyo mwenye miaka 32 ameweka rekodi ya kutohama Barcelona tangu ajiunge nayo mwaka 2003.

Messi amefanikiwa kufikisha michezo 700 ndani ya Barcelona na kufunga mabao 609 kwa kuikaribisha Borrusia Dortmund mchezo uliochezwa uwanja wa Nou Camp  na akifanikiwa kufunga bao la pili dakika ya 33 kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Barcelona kushinda mabao 3-1 huku Suarez akifunga bao la kwanza dakika ya 29 na Antonio Griezman akifunga bao dakika ya 65.

Kwa upande wa Barcelona Messi ameendelea kuandika vitabu vya kihistoria kama mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi na kwa mafanikio zaidi klabuni hapo. Mpaka sasa Lionel Messi anaongoza kwa kuwa na magoli mengi Barcelona na ametwaa tuzo nyingi zaidi ndani ya klabu hiyo kuliko mchezaji yeyote aliyewahi kucheza klabuni hapo.

Post a Comment

0 Comments