BETI NASI UTAJIRIKE

KWELI SIMBA YA KIMATAIFA ,YAINYUKA YANGA 3-0

Klabu ya Simba imeendelea kujitangaza zaidi Afrika na duniani kwa kufanikiwa kutoa wachezaji watatu waliowahi na wanaoichezea timu hiyo kwenye tuzo za CAF


Simba imemtoa Emanuel Okwi (aliichezea klabu hiyo kwa mafanikio makubwa msimu wa 2018/19) na baadaye aliondoka klabuni hapo na kuelekea  Uarabuni. Okwi ni mmoja wa wachezaji muhimu walioisaiia klabu hiyo kufika robo fainali ligi ya Mabingwa Africa kwa msimu wa 218/19 na ameteuliwa kuwania tuzo za mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Mbwana Samatta aliwahi ichezea klabu ya Simba kwa mafanikio makubwa sana na kupitia klabu hiyo alifanikiwa kusajiliwa TP mazembe na baadaye kutua KRC Genk. Tangu akiwa TP Mazembe alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi za ndani na sasa anakibarua kikubwa baada ya kutajwa kuwania tuzo za mchezaji bora Afrika akipambana na akina Mo Salah 


Meddie Kagere ndiye straika hatari zaidi kwa sasa Tanzania akiwa na jumla ya magoli 8 kwenye ligi kuu Tanzania bara,. Kagere ameingia kwenye listi ya wchezaji 20 wanaowania tuzo za CAF kwa mchezaji bora kwa ligi za ndani akiwa ameiisaidia Simba kufika robo fainali msimu wa 2018/19

Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kutoa wachezaji ndani ya orodha hiyo CAF wanaowania uchezaji bora ndani ya bara la Afrika ambapo wamewafunika watani zao wa jadi Yanga ambao hawajafanikisha hilo.

Yanga haina historia ya kumtoa mchezaji yeyote aliyewahi kugombea tuzo hizo kubwa Afrika .

Post a Comment

0 Comments