advertise with us

ADVERTISE HERE

KOCHA YANGA AENDELEA KUONYESHA UDHAIFU WA MWINYI ZAHERA

Kocha Boniface Mkwasa ameendelea kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwa kikosi cha Yanga kilichoonekana dhaifu enzi za Papa Mwinyi Zahera . Mkwasa ameanza kujizolea sifa



kem kem baada ya Yanga  kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa kirafiki jioni ya jana Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.


Haukuwa ushindi mwepesi katika mchezo wa nne kwa kocha Charles Boniface Mkwasa tangu arithishwe mikoba ya Mkongo Mwinyi Zahera, kwani Yanga ililazimika kutoka nyuma kwa bao 1-0 kipindi cha pili.

Beki Ally Abdulkarim Mtoni ‘Sonso’ aliye katika msimu wake wa kwanza Jangwani tangu awasili kutoka Lipuli FC ya Iringa alijifunga dakika ya 44 akijaribu kuokoa krosi ya Said Mudathir.
Kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfna Ngassa akaifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 70 kwa shuti la mbali mkongwe huyo akimalizia pasi ya Mnamibia Sadney Urikhob.

Ngassa alifunga bao hilo mshambuliaji Mkongo, David Molinga ‘Falcao’ akitoka kukosa penalti baada ya Abubakar Nyakarungu kuunawa mpira kwenye boksi.  Kiungo Mkongo Papy Kabamba Tshihismbi akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 90 na akiiwahi krosi ya Mapinduzi Balama baada ya kuvunja mtego wa kuotea wa mabeki wa Coastal Union na kumchambua kipa Abubakar Abbas kiulaini. 
Mshambuliaji Juma Balinya akaifungia Yanga SC bao la tatu dakika za nyongeza kwa penalti baada ya beki wa Coastal Union Ibrahim Ame kuushika mpira kwenye boksi kufuatia shuti la Mganda huyo aliye katika msimu wake wa kwanza Jangwani tangu awasili kutoka Polisi ya Kampala.
Huo ulikuwa mchezo wa nne kwa Mkwasa aliyerejeshwa mwanzoni mwa mwezi huu kama kocha wa muda baada ya kufukuzwa Zahera, akiwa ameshinda tatu nyingine 1-0 dhidi ya Ndanda FC Ligi Kuu na 5-0 dhidi ya Kombaini ya Nanyumbu, kabla ya kufungwa 1-0 na Mkuti Market zote za kirafiki mkoani Mtwara. 

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Farouk Shikalo, Juma Abdul, Jaffar Mohammed, Mustafa Suleiman, Ally Mtoni ‘Sonso’, Papy Tshishimbi, Said Mussa/Mrisho Ngassa dk46, Raphael Daudi/Juma Balinya dk56, David Molinga/Adam Kiondo dk76, Sadney Urikhob na Mapinduzi Balama.

Coastal Union; Abubakar Abbas, Ayoub Masoud, Omar Salum, Ibrahim Ame, Abubakar Nyakarungu, Salum Ally, James Kahimba/Ayoub Semtawa dk77, Exavery Chahenge, Mudathir Said, Deogratius Anthony, Mohammed Mussa/Hijja Ugando dk56.

Post a Comment

0 Comments