advertise with us

ADVERTISE HERE

KOCHA WA SIMBA AWAPOTEZEA KMC,APEWA DILI NONO ZAIDI

Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba Masoud Djuma amefuta tetesi zilizoenea kuwa anarejea nchini Tanzania kunoa kikosi cha KMC 


Taarifa zilienea hivi karibuni kuhusiana na ujio wa kocha huyo kwnye klabu ya KMC. Kwa sasa kocha huyo ataendelea kubaki Rwanda kuifundisha klabu ya Bugesera inayoshiriki ligi kuu Rwanda kwa kipindi cha miezi 6 na baada ya hapo ataweza oondoka au kuongeza mkataba na hiyo itategemea amefanyaje kwa nusu msimu uliobaki wa ligi hiyo.

Klabu hiyo imeanza vibya msimu huu wa Ligi kuu Rwanda baada ya kucheza michezo 8 ikishinda michezo 2 ,Sare 2 na kupoteza michezo 4. Kwa matokeo hayo klabu hiyo inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 8.Kocha masoud Djuma anapaswa kuonyesha uwezo wake wa hali ya juu kuinusuru timu hiyo isishuke daraja msimu huu kwenye ligi kuu Rwanda yenye timu 16 tu.,


Post a Comment

0 Comments