Klabu ya Prisons Tanzania imeendelea kuwa tisho kwa vigogo wa ligi kuu Tazania baada ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi kuu tangu uanze msimu wa 2019/20
Ilitarajiwa Prisons Tanzania ingefungwa kwa mara ya kwanza na Simba lakini mambo yalikuwa ni tofauti na matarajio ya mashabiki wa Msimbani baada ya timu hiyo kulazimishwa suluhu ya mabao 0-0 na kuifanya Prisons kutopoteza mchezo wowote kwa msimu wa 2019/20
Baada ya mchezo huo kocha wa Polisi Tanzania alinukuliwa akisema
"Tumecheza na timu nzuri ,ina uwezo na mipango mizuri na vijana wazuri,ukiangalia timu tuliyocheza nayo ina wachezaji 7 timu ya taifa wakati sisi tunamchezaji 1 tu timu ya Taifa kwahiyo unaweza kuona ubora. Tulikuwa tunacheza na timu ambayo tulipaswa kuchukua tahadhali muda wote wa mchezo, Nidhamu yetu ya kuzuia ilikuwa nzuri sana na imetusaidia kwani pointi 1 kwa gemu kubwa kama hii ni sawa"
Kwa matokeo hayo Prisons imejikusanyia pointi 16 ikicheza michezo 10 na kuwa nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu.
0 Comments