BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA MKUU TAIFA STARS ATOA SABABU ZA MANULA KUTOITWA KIKOSINI

Kocha mkuu wa Taifa Stars Mrundi Etienne Ndayiragije  amefanya mazungumzo na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Equatorial Guinea



Kocha huyo amezungumzia mambo mengi kuhusiana na mchezo huo utakaopigwa hapo baadaye na amenukuliwa akisema 

"Tumejianda vizuri na wale wote tuliowata wakovizuri hakuna shida na morali ya timu iko vizuri, tunashukuru Mungu kwani mpaka sasa maandalizi yanaendelea na tunaimani kuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutapata matokeo mazuri.

Tunahitaji kwenda tena AFCON na tumejiandaa kwani tunafahamu ushindani ni mkubwa na tumejiandaa kumaliza vizuri. La msingi  ni kuhakikisha tunafuzu , kutoka mwanzo tulipanga  kuhakikisha tunafuzu.


Mabadiliko kwenye kikosi ni jambo la kawaida kwa sababu hii ni timu ya nchi na tunapanga kutokana na kile tunachoona kitatupa manufaa kwa sasa. Na kama isingekuwa kubadili wachezaji basi tusingekuwa tunafanya mazoezi  tungekuwa tunakutana siku ya mechi tu na kuingia uwanjani. Ikiwa tunajiandaa kutokana na aina ya wapinzani wetu wako vipi na tunahitaji kupata matokeo basi ni muhimu kufahamu nani yuko tayari kwa wakati huo ili kuhakikisha timu inafuzu"


Mchezo huo utapigwa  saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam na unatarajiwa kuleta matokeo chanya kwa Taifa Stars inayopigania nafasi ya kufuzu michuano ya AFCON 2021.  Viingilio vya mchezo huo ni shilingi 3000 na elfu 5000 kwa jukwaa kuu huku wadau mbalimbali wakiombwa  kujitokeza kuishangilia timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments