BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU NDIYE MCHEZAJI BORA KIJANA MWAKA 2019

Kiungo mchezeshaji wa Atletico Madrid Joao Felix ametajwa kama mchezaji bora kijana kwa mwaka 2019 akiwapita Jadon Sancho wa Borrusia Dortmund na Elrng Hooland 
wa Red Bull Salzburg. Joao Felix mwenye thamani ya Dola milioni 146 alinunuliwa na Atletico Madrid akitokea Benfica mwezi July mwaka 2019 na kufanikiwa kucheza michezo 13 kwenye michuano yote akifunga mabao 3.

Joao mwenye miaka 20 alifikia thamani hiyo baada ya kufunga mabao 15 ndani ya Benfica na kuchangia upatikanaji wa mengine 7 ndani ya klabu hiyo kwa msimu wa 2018/19.

Kutwaa kwa tuzo hiyo kutamfanya Joao Felix awekwe kundi moja washindi waliopita akiwemo Paul Pogba ,Lionel Messi ,De Ligt na Mbappe. Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo na Tuttosportz Felix alinukuliwa akisema 

" Nawashukuru Tuttosport kwa tuzo hii ya mchezaji bora  kijana kwa mwaka 2019. Mimi ni mchezaji wa pili wa Atletico Madrid kushinda tuzo hii na nina furaha

"Naishukuru klabu ya Benfica pamoja na kocha Bruno Lace  kwa mengi aliyoyafanya kwangu na Familia yangu na nyakati zote alikuwa karibu yangu.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Jadon Sancho wa Borussia Dortmund na timu ya taifa Uingereza. Sancho alitajwa kama mchezaji bora kijana wa kiingereza siku chache zilizopita baada ya kuwa na mchango mkubwa kwenye timu ya taifa hilo.

Kai Havertz wa Bayern Leverkusen alishika nafasi ya tatu akimpiku mshambuliaji Haaland aliyeshika nafasi ya nne huku De Ligt kishika nafasi ya 5 kwenye tuzo hizo.

Post a Comment

0 Comments