advertise with us

ADVERTISE HERE

KINONDONI MUNICIPAL COUNCIL (KMC) YAMGEUKIA NYOTA WA SIMBA

Klabu ya Kinondoni Municipal Council inayomilikiwa na Manispaa ya  kinondoni Jijini Dar es salaam imeigeukia klabu ya Simba na kumuhitaji nyota wake Rashid Juma.


Nyota huyo amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao watetezi na klabu mbalimbali zikiwemo Polisi Tanzania na KMC zimeonyesha kumhitaji.

Mchezaji huyo amebakiza mwaka mmoja tu kuitumikia klabu hiyo na kama atabakizwa klabuni hapo basi ataondoka bure mwishoni mwa msimu wa 2019/20 kitu ambacho Simba hawatakubali na wamepanga kumtoa kwa mkopo huku wakimuandalia kataba mnono endapo atafanya vizuri.

Bodi ya ligi imetangaza kufungua dilisha dogo la usajili kuanzia tarehe 15 Novemba mpaka 15 Disemba na hii ni nafasi pekee kwa mchezaji huyo kuhamia kwenye moja ya klabu hizo na kuendeleza kiwango chake 

Post a Comment

0 Comments