Kuelekea mchezo huo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wamejiandaa vizuri.
Kauli hiyo imekuja ambapo hivi sasa Yanga tayari wameshatua Misri kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itakuwa ya kupindua matokeo kufuatia kupoteza kwa mabao 2-1 hapa nyumbani.
Mwakalebela ambaye tayari alishatua Misri mapema kabisa kwa ajili ya maandalizi ya kuipokea timu, ameeleza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na watapambana kupata matokeo.
Ameeleza wana matumaini ya ushindi baada ya kugundua kuwa huko Misri Pyramds inazungumziwa kama timu ya kawaida suala ambalo amelisema linawapa nguvu.
"Unajua hapa Misri Pyramids wanaisema kuwa ni timu ya kawaida kabisa, hivyo inatupa nguvu kuelekea mechi ya marudiano, naimani tutafanya vizuri ikiwemo kupindua matokeo," amesema.

Baada ya kauli hiyo mashabiki wa Yanga wameonekana kufurahishwa na wanaamini wataashinda mchezo huo kiurahisi. Yanga inatakiwa ishinde mabao 2-0 au 3-1 kuweza kufuzu makundi.
0 Comments