BETI NASI UTAJIRIKE

KAPTENI WA SIMBA ATANGAZA VITA KWA WAPINZANI LIGI KUU

Mshambuiaji hatari wa Simba John Bocco amekwishapona majeraha na sasa anarejea dimbani rasmi. Mshambuliaji huyo amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili 


akisumbuliwa na majeraha ya mguu wake. Taarifa za kuaminika zinasema Bocco amekwisha pona na kunachosubiriwa ni kupewa mechi tu.

 John Bocco, ameweka wazi kwamba pacha yake na Meddie Kagere itafunga mabao mengi. Bocco amesema hayo licha ya kwamba hadi sasa bado hajacheza hata mechi na Kagere kutokana na kuwa majeruhi.

Bocco na Kagere kwa sasa ndiyo wanatazamiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba katika michezo ya ligi ikiwa baada ya kucheza sambamba tangu msimu uliopita.

Straika huyo ameliambia amospoti.com , kuwa licha ya kwamba wameshindwa kucheza sambamba yeye na Kagere hadi sasa lakini anaamini atakaporudi na kuunganisha pacha hiyo watazisumbua timu nyingi za ligi kuu.

“Kitu kibaya ni kwamba hadi sasa mimi na Kagere hatujacheza sambamba pamoja tukiwa wawili. Tulicheza msimu uliopita lakini tulikuwa watatu mimi, Kagere na Okwi kwa hiyo ikatunyima nafasi ya kucheza sambamba.

“Niseme tu wazi kuwa naona kabisa tutasumbua wakati ambao tutacheza pamoja nikitoka katika majeruhi ambayo yamechangia kwa kiwango kikubwa kutocheza hadi sasa katika timu,” alisema Bocco.

Post a Comment

0 Comments