advertise with us

ADVERTISE HERE

KAPTENI MBWANA SAMATA AUZUNGUMZIA MCHEZO UNAOFUATA DHIDI YA LIBYA

Kapteni wa Timu ya Taifa Tanzania na Klabu ya Genk ameuzungumzia mchezo unaofuata dhidi ya Libya utakaopigwa siku ya jumanne tarehe 19. Awali timu hiyo ilipanga kuondoka 


kuelekea Tunisia siku ya jumapili ila imelazimika kuondoka usiku wa jana mara tu baada ya kumaliza mchezo wake dhidi ya Equatorial Guinea waliopata ushindi wa mabao 2-1 huku mabao ya Taifa Stars yakifungwa na Msuva na Sure boy.

Akiwa uwanja wa ndege Julias Nyerere International Airport Samatta alinukuliwa na wanahabari akisema :

"Mimi nafikiri tuanze kucheza kama tulivyocheza mpira wa leo(jana) dhidi ya Equatorial Guinea kwamba tusisubiri mpaka dakika salama au wapinzani wetu  wakiwa wamepata goli. Kama tumeanza vyema mchezo wa leo nina uhakika itazidi kufanya vizuri zaidi na tulistahili kupewa penati ila refa hakuiona ila kama watarudia video basi naamini wataona " 

Taifa Stars inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lao ikiwa na pointi 3 na goli moja huku Tunisia ikiongoza kundi kwa pointi 3 na mabao 3.

Post a Comment

0 Comments