ads

adds

JESHI LA KUIANGAMIZA EQUATORIAL GUINEA NA LIBYA LAENDELEA NA MAZOEZI, YUPO PIA ALIYEWAFUNGA LIVERPOOL

Nahodha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Mbwana Samatta amekwisha kujiunga na Kambi ya Kikosi hicho kujiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Equatorial Guinea 

Mchezo huo utachezwa siku ya Ijumaa hii Novemba 15 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam maarufu kama kwa mkapa .Samatta anayecheza KRC Genk ya Belgium anatarajia kuiongoza Taifa Stars kwa mchezo huo dhidi ya Equatorial Guinea na mchezo utakaofuata siku 4 baadaye dhidi ya Libya utakaochezwa ugenini.
Wachezaji wengine wanaocheza nje ya Tanzania waliokwisha kuwasili jana usiku ni Farid Mussa anayecheza Tenerife ya Hispania na Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadid ya Morocco.
Wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania ambao tayari wameripoti Kambini ni David Kisu(Gor Mahia,Kenya),Ramadhan Kessy (Nkana,Zambia) na Eliuter Mpepo (Buildcon,Zambia)
Taifa Stars tayari imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ikipiga Kambi kwenye Hoteli ya Blue Saphire,barabara ya Pugu.
Mchezo dhidi ya Equatorial Guinea utachezwa saa 1 usiku Uwanja wa Taifa Ijumaa Novemba 15.Kiingilio kwenye mchezo huo ni shilingi 3,000 mzunguko,5,000 VIP B na C

Post a Comment

0 Comments