ads

adds

JE HUU NI MWISHO WA RONALDO ? FABIO CAPPELO NA SARRI WATOA NENO

Mshambuliaji mahili wa Juventus na Ureno ameendelea kukalia kuti kavu msimu huu baada ya kutokuwa na mwanzo mzuri kwenye  mechi za Serie A na UEFA msimu huu. 


Hapo jana Ronaldo alitolewa uwanjani dakika ya 55 baada ya kushindwa kuonyesha uwezo wake kwenye mchezo wa Serie A dhidi ya AC Milan na baada tu ya kutolewa alielekea chumba cha kubadilishia nguo pasipokuzungumza na mtu yeyote na alionekana kukasirika.

Nafasi ya Ronaldo ilichukuliwa na Dybala ambae aliipa Juventus bao la ushindi dakika ya 77 kwenye mchezo huo na kuifanya Juventus ibai kileleni mwa ligi hiyo.

Aliyewahi kuwa kocha wa Uingereza, Mchezaji wa Italy Fabio Capello na sasa ni mtangazaji wa Serie A alisikika akisema Cristiano hajafanikiwa kupiga chenga na kumpita beki yeyote kwa kipindi cha miaka 3. Capello alinukuliwa akisema 

"Sijapenda na sijafurahishwa na mchezaji mkubwa kama yeye kutolewa nje ya uwanja kisha kuelekea vyumbani moja kwa moja badala ya kukaa benchi akiwatazama wenzake"

" Ukweli ni kwamba Ronaldo hajafanikiwa kuwapiga chenga wapinzani na akafunga kwa kipindi cha miaka 3. Nimefanya utangazaji nikiwa La Liga na nakumbuka mambo mengi aliyokuwa anafanya kwa wapinzani ila si kwa sasa"

"Ronaldo ni mchezaji mzuri na ana rekodi nyingi sana lakini kwa sasa kuna Dybala na Douglas Costa ambao wanafanya mambo mazuri ndani ya klabu hasa kufunga mabao mazuri , kasi waliyonayo na uwezo wa kupiga chenga vinawafanya wawe tofauti na Ronaldo"

"Juventus wanaonekana wanamtegemea yeye zaidi ilihali wana wachezaji wengi wazuri mfano leo bila Ronaldo wameshinda mchezo wao" alimaliza hivyo Fabo Capello.

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa klabu hiyo Maurio Sarri aliibuka na kumpongeza nyota huyo kwa kucheza vizuri ilihali anamajeraha mguuni. Sarri alinukuliwa akisema 

"Tunatakiwa kumshukuru Ronaldo kwa kujitolea kwake kwenye mchezo huu maana alikuwa anasumbuliwa na mguu. Alijitahidi kucheza inavyopaswa lakini niliona hayuko sawa hivyo niliamua kumtoa,. Ni kawaida kwa mchezaji kutoka moja kwa moja bila kwenda benchi baada ya kutolewa uwanjan hasa anapokuwa na majeraha"



Post a Comment

0 Comments