advertise with us

ADVERTISE HERE

IFAHAMU MIAKA 17 YA RONALDO NDANI YA JEZI YA URENO

Mchezaji mahili duniani Cristiano Ronaldo ameendelea kuzeeka taratibu na kiwango cha hali ya juu. Kama umemfuatilia mchezaji huyo toka mwaka 2003 mpaka 2019 utanielewa namaanisha nini hasa kwa uwezo wake wa kufunga . Wengi wenu mmemfahamu Ronaldo akiwa Manchester United ila binafsi nimemfahamu akiwa Sporting Lisbon. Cristiano amecheza michezo 164 akiwa na jezi ya Ureno na amekuwa mchezaji bora wa taifa hilo kwa miaka 12 mfululizo. 

Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kwenye orodha ya wafungaji bora wa timu ya taifa  Ureno akiwa na mabao 99 kwenye michezo 164 huku akitegemewa kuvunja rekodi ya mfungaji bora wa muda wote mwenye mabao 109  na kuwa mfungaji bora kwa timu za taifa.

Ukiwataja nyota watano wakubwa kwa taifa la Ureno basi ni lazima Uanze na nyota huyo mwenye Ballon D' Or 5 alizobeba mwaka 2009,2013,2014 , 2016 na 2017 huku akiisaidia ureno kutwaa makombe mawili makubwa ya Ulaya. Nyota wengine ni Eusebio ,Luis Figo na Paul Futre

Tangu Ronaldo aitumikie Ureno ameiwezesha timu hiyo kucheza kombe la dunia mara 4 mfululizo toka mwaka 2006,2010,2014 na 2018 pia anategemewa kuivusha timu hiyo kuelekea nchini Qatar mwaka 2022.

REKODI YA RONALDO TANGU MWAKA 2003-2019


Post a Comment

0 Comments