BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU NDIYE KOCHA MPYA WA TOTTENHAM HOTSPUR

Klabu ya Tottenham imetangaza kumpata kocha mpya baada ya kumtimua aliyekuwa kocha  wake mkuu kwa miaka mitano Mauricio Pochettino.

Shida imerejea tena ligi kuu Uingereza baada ya Jose Mourinho kukabidhiwa rasmi mikoba ya kukinoa kikosi cha Tottenham chenye makao yake makuu London.

Mourinho anachukua nafasi ya muargentina Mauricio Pochettino aliyetimuliwa jana na klabu hiyo  kwa kile kinachodaiwa ni mwenendo mbovu wa klabu kwenye michuano mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi kuu Uingereza. 

Mourinho amelamba dili la kuifundisha klabu hiyo kwa misimu mitatu mpaka msimu wa 2022-23.Kocha huyo amefanya kazi na klabu nguli kama Manchester United na Chelsea na ameziwezesha kutwaa makombe mbalimbali.

Mwenyekiti wa Spurs Dniel Levy alinukuliwa akisema " Tumefanikiwa kuwa na Jose ambaye ni kocha mwenye mafanikio makubwa kwenye soka "

Naye Jose Mourinho alinukuliwa akisema "Ubora wa kikosi na akademi vinanifurahisha , kufanya kazi na wachezaji hawa ni jambo lililonivutia"

Post a Comment

0 Comments