BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU NDIYE ALIYETAKA KUMHARIBIA KAZI PATRICK AUSSEMS KWA SIMBA

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Patrick Aussems alihusishwa na kutimuliwa klabuni hapo baada ya kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na klabu hiyo. Baada ya uchunguzi 


wa kina amospoti.com ilipata jibu na inatajwa kuwa Mkude amemponza Aussems kutokana na kocha huyo kuwa na urafiki wa karibu na kiungo huyo kiasi cha kutompa adhabu anapofanya vitendo vya utovu wa nidhamu ambavyo vinajirudia.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ambavyo viko ndani ya Simba, Mkude ni moja ya sababu ya kutimuliwa kwa Aussems kutokana na aina ya malezi ambayo kocha huyo alikuwa anampa kiungo huyo.



Kocha huyo amekuwa akimbeba mara kadhaa kiungo huyo wakati ambao anafanya makosa.Alimuacha bila ya kumchukulia adhabu yoyote wakati ambao alifanya makosa ya nidhamu wakati wa safari ya Kagera na Mara wakati wa mechi dhidi ya Biashara United na Kagera Sugar.

“Lakini pia hivi karibuni wakati ambao alitimuliwa timu ya taifa katika mechi dhidi ya Equatorial Guinea alikaa nyumbani na kutokuja katika timu hadi wakati ambao wenzake ambao walikuwa timu ya taifa waliporudi naye ndiyo akarudi nao.

“Aliporudi kambini kocha akataka kumpanga kwenye mechi iliyofuata lakini viongozi wakagoma na kumwambia anatakiwa akakae jukwaani kwa sababu hakuwa amefanya mazoezi na timu.

“Lakini pia kumekuwa na makosa mengi ambayo kiungo huyo aliyafanya na bado kocha alimuacha bila ya kumchukulia hatua zozote zile za kinidhamu licha ya kwamba tayari alikosea,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mmoja wa vigogo wa klabu hiyo.

Kuweka mzani sawa amospoti.com, ilimtafuta Katibu wa Simba, Dk Anord Kashembe kuzungumzia hilo ambapo alisema:

Juu ya hilo la adhabu zinazochukuliwa kuna kamati ya maadili ambayo ndiyo inadili na kila kitu. Wao ndiyo wanatoa maamuzi kwa wachezaji wote ambao wanafanya utovu wa nidhamu, labda mseme mnataka kwa namna gani tutoe adhabu kwa wachezaji hao?”

Post a Comment

0 Comments