BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU HAPA ALIYECHUKUA NAFASI YA CHARLES BONIFACE MKWASA YANGA


Uongozi wa Klabu ya Yanga umemtangaza rasmi David Ruhago kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo kuanzia leo tarehe 11/11/2019.


Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Yanga, imesema uteuzi huo umefanywa na kamati yake ya utendaji chini ya Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla.Ruhago amekuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za Yanga katika vipindi tofauti.


Katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja tangu kuondoka madarakani aliyekuwa Katibu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa, nafasi hiyo imekaimiwa na viongozi watatu tofauti ambao ni Omar Kaya, Dismas Ten na Thabit Kandoro aliyekaimu nafasi hiyo kwa siku 11 pekee tangu Novemba 1, 2019.

Post a Comment

0 Comments