advertise with us

ADVERTISE HERE

HUU NDIO UKWELI KUHUSU KOCHA PATRICK AUSSEMS KUONDOKA SIMBA

Mashabiki wa klabu ya Simba wamepigwa na butwaa siku ya leo baada ya kusikia kocha wake mkuu Patrick Aussems ameondoka nchini kurejea Ubelgiji Taarifa ya chombo kimoja cha habari ilileta mkanganyiko na kuibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki waliodhani kocha huyo ameondoka moja kwa moja. 

Amospoti.com ilizinyaka taarifa hizo na kuingia chimbo kutafuta ukweli wa habari hiyo, Chombo hicho kilichapisha habari yenye kichwa cha habari iliyosomeka "AUSSEMS AKACHA MAZOEZI SIMBA SC, ATIMKA KWAO" na kwa umakini mkubwa wahariri wetu waliipitia habari ile na kubaini kuwa ni kweli Aussems ameondoka nchini Tanzania leo asubuhi  kwa sababu za kifamilia nchini Ubelgiji na atarejea siku chache zijazo kabla ya mechi na Ruvu shooting.

Moja wa viongozi wa Simba alinukuliwa akisema " Aliniambia asubuhi kwamba hataweza kufika mazoezini, atalazimika kusafiri na atakuwa huko kwa siku zaidi ya tatu ili kumaliza matatizo yake hayo kwa maana tunategemea kuwa naye hapa siku ya Alhamisi"

Amospoti.com inawakumbusha watanzania wote kuwa makini na usomaji wa habari nzima na si kuishia kujaji wasomapo kichwa cha habari.


Post a Comment

0 Comments