BETI NASI UTAJIRIKE

HIZI NDIZO SABABU TATU ZA SIMBA KUMPIGA BENCHI KOCHA AUSSEMS

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba alithibitisha kutokuwepo kwa kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems kwa kile kinachodaiwa ni kuzuuiwa na mabosi wa klabu hiyo kwa muda 


usiojulikana .imeripotiwa kuwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems tangu mechi ya Ruvu Shooting amesimamishwa kufanya kazi yoyote ndani ya klabu hiyo.

Taarifa imesema maamuzi hayo yamekuja kufuatia makosa mbalimbali aliyoyafanya Aussems ndani ya timu ikiwemo la kuondoka nchini bila ruhusa ya mabosi wake.

Mbali na kuondoka bila ruhusa, inaelezwa pia Aussems aligoma kukaa kitako na Ofisa Mtendaji wa klabu, Senzo Mazingisa ambacho kililenga kujadili mambo kadhaa kuhusu timu siku chache zilizopita.

Ukaichana na sababu tajwa hapo juu, inaelezwa pia kuwa uwezekano wa Aussems kuondoshwa ndani ya Simba upo kutokana na mwenendo wa kikosi cha timu ulivyo.

Inavyosemekana ni kuwa Aussems amekuwa na urafiki uliopitiliza na wachezaji kiasi cha kwanza inapelekea baadhi ya wachezaji kuwa na changamoto ya nidhamu jambo ambalo limechukuliwa kitofauti.

Post a Comment

0 Comments