BETI NASI UTAJIRIKE

HIVI NDIVYO OLE GUNNAR NA UNAI EMERY WANAVYOWATESA WENGER NA FERGUSON

Makocha wa klabu za Arsenal na Manchester United Unai Emery na Ole Gunnar wameendelea kufanya vibaya msimu huu baada ya kukubali vipigo kwenye


 michezo ya Europa League. Makocha hao wameshinda kufanya vizuri ligi kuu England kwa Arsenal kushika nafasi ya 8  ikiwa na pointi 18 huku Manchester United ikiwa nafasi ya 9  na pointi 17.

Arsenal.
Klabu hiyo imecheza michezo 13 ya Premier League na kushinda michezo 4 huku  ikitoka sare michezo 6 na kufungwa 3. Arsenal imefunga mabao 18 tu na kufungwa mabao 19

Kwa upande wa Europa league Arsenal wamecheza michezo 5 ya kundi F huku wakishinda michezo 3 sare 1 na kufungwa 1 na wanaongoza kundi Hilo kwa points 10 wakifunga mabao 12 na wakifungwa mabao 5 pekee.


Manchester United
Klabu hiyo imecheza michezo 13 ya premier league na kushinda michezo 4 sare 5 na kufungwa michezo 4.Manchester united imefunga mabao 19 na kufungwa mabao 15

Kwa upande wa Europa league Manchester United imecheza mechi 5 za kundi L ikishinda michezo 3 sare 1 na kufungwa 1 na wanaongoza kundi hilo kwa pointi 10 wakifunha mabao 6 na kufungwa mabao 2 pekee.

Klabu hizo zimefuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo na kinachosubiriwa kwa Sasa ni mechi za mwisho.

usiku wa Jana klabu hizo zilipoteza tena michezo ya Europa kwa Manchester United kufungwa mabao 2-1 na Astana huku Arsenal akifungwa 2-1 na Eintracht

Kwa msimu wa 2019/20 unai Emery na Ole Gunnar walikutana tarehe 30 septemba kwenye mchezo wa premier league uliomalizika kwa sare ya mabao 1-1

Makocha wa zamani wa timu hizo Arsene Wenger na Alex Ferguson wamejikuta wakipata wakati mgumu kutazama mechi za timu hizo kutokana na matokeo hayo mabovu kwa timu hizo

Post a Comment

0 Comments