ads

adds

HIVI NDIVYO MOHAMMED DEWJI ANAVYOWAMALIZA YANGA KWA PRESHA,MANJI AKUMBUKWA

Unakumbuka Enzi za Manji pale Yanga?Unakumbuka mwenyekiti yule alivyokuwa anafanya kufuru kwenye sajili za wachezaji klabuni pale. Tanzania hakukuwa na mtu kama Manji 



kwa kufuru alizokuwa anazifanya klabuni hapo. Manji alikuwa kila kitu ndani ya Yanga kuanzia Usajili ,Mishahara na hata matumizi yote ya klabu ile. Nakumbuka wakati Yusuf Manji anaingia klabuni pale alipaka rangi majengo ya Yanga, aliboresha gym ya Yanga ,aliwalipa wachezaji wote na viongozi mishahara minono na hakuna mchezaji aliyetaka kwenda kucheza nje ya Yanga . 

Swali ni nini kilitokea pale Yanga?

Wakati Yusuf Manji anaendelea na majukumu yake kama mwenyekiti aliwaomba wanachama wamkodishe klabu hiyo kwa miaka kumi ndipo ugomvi ulipoanzia. Kuna watu walimuunga mkono lakini kuna baadhi walimkejeli na kusema suala hilo haliwezekani.

 Muda mfupi baadaye Yusuf alipata tuhuma mbalimbali  kutoka serikalini ndipo mambo yalipoanza kuharibika. Nafasi ya Manji ilikaimiwa na Clement Sanga aliyekuwa makamu Mwenyekiti wa Yanga. Mbali na juhudi zake za kiuongozi hasa kutaka kuleta mfumo mpya wa uendeshaji bado alionekana hafai na walimtaka aachie ngazi klabuni hapo na alifanya hivyo.

Wakati hayo ya Yanga yanatokea je Simba walikuwa wapi?

Wakati migogoro ya Yanga ikipamba moto klabu ya Simba ilishaanza mipango ya kubadili uendeshaji wa klabu. Mbali na kwamba zoezi hilo kuwa gumu lakini lilifanikiwa vyema mwaka 2018 na klabu hiyo kuanza kuendeshwa kwa mfumo wa kisasa chini ya mwekezaji Mohamed Dewji mwenye asilimia 49 huku wanachama wakimiliki asilimia 51.

Matokeo ya maamuzi kati ya viongozi wa Simba na Yanga

Yanga walikataa mfumo mpya wa kiuendeshaji na wakaamua kuachana na Manji.Mwaka 2018 klabu hiyo ilikumbwa na njaa kali na kuanza kutembeza bakuli huku nyota wake kama Gabriel Michael,Kakolanya ,Ajib wakitimka klabuni hapo.Mbali na hayo tumeshuhudia timu hiyo ikidaiwa mahotelini ,wachezaji kula mlo mmoja na wakati mwingine kumtegemea aliyekuwa kocha wa kikosi hicho mwinyi Zahera kuwa mfadhili.  

Simba waliukubali mfumo mpya na sasa tunaona matunda yake kwani wachezaji wanalipwa vizuri ,wanasajili vizuri na sasa mwekezaji wa klabu hiyo anakamilisha ahadi yake ya ujenzi wa viwanja viwili vya mazoezi ambavyo klabu hiyo imeshindwa kuvijenga kwa zaidi ya miaka 83 toka kuanzishwa kwake. Tumeshuhudia timu hiyo ikifika robo fainali ligi ya mabingwa Afrika na hizo zote ni juhudi za mfumo mpya wa kuendeshaji

Hali ilivyo Yanga 

Klabu hiyo inahali mbaya kiuchumi na imefikia hatua inaanza kumtafuta mchawi ni nani kati ya Viongozi,wachezaji na kocha. Yanga wanatamani Manji arudi , Yanga wanatamani wabadili mfumo wa kiuendeshaji. Yanga inawanachama wenye nguvu kama Rostam Aziz na Ghalib Muhammed (GSM) na inaweza watumia watu hao kama wawekezaji wa muda ili waweze kukamilisha mabadiliko ya mfumo mpya.

Swali ni je nani wa kuwekeza klabuni hapo kwa mfumo huo wa kizamani? Viongozi wa Yanga wanapaswa kukaa chini na kuzungumia suala hilo kwa ufasaha huku wakiiga mfumo wa Simba au kuja na mfumo wao mpya. kama wataapuuza hayo kwa sasa basi watakuja kumbuka kuvuta shuka asubuhi na Simba itakuwa imewaacha mbali mno.

Post a Comment

0 Comments