advertise with us

ADVERTISE HERE

HII HAPA TAREHE YA MCHEZO KATI YA BARCELONA NA REAL MADRID (EL CLASSICO)

Chama cha soka Uhispania kimetangaza rasmi tarehe kamili ya mchezo wa ligi kuu "LA LIGA " kati ya Barcelona na Real Madrid maarufu kama El ClassicoMchezo huo utapigwa tarehe 18 Disemba 2019 jijini Catalunya na uwanja wa Nou Camp . Mchezo huo uliahirishwa  kutokana na maandamano yakimapinduzi yaliyokuwa yaendelea jijini Catalunya. 

Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa tarehe 26 Oktoba ila kwa sababu hizo uliahirishwa na kusogezwa mbele. Chama cha soka Hispania kilikubali maombi ya vilabu hivyo kuucheza mchezo huo tarehe 18 Disemba badala ya 7 Disemba iliyopangwa na La Liga.

Barcelona na Real Madrid zinalingana pointi baada ya kucheza michezo 12 na zote kuwa na pointi 25 huku Barcelona ikiongoza kwa magoli.

Atletico madrid inashika nafasi ya tatu ikiwa imecheza michezo 13 mmoja zaidi ya Barcelona na Real Madrid na kujipatia pointi 24.

Post a Comment

0 Comments