BETI NASI UTAJIRIKE

HII HAPA RATIBA NZIMA YA CECAFA

Shirikisho la Soka Africa mashariki na kati ( Council of East and Central Africa Football Association "CECAFA" limetangaza rasmi ratiba ya michuano hiyo kwa mwaka 2019 

Huku Kilimanjaro Stars (Tanzania Bara) wamepangwa Kundi C kwenye michuano hiyo.
Kilimanjaro Stars wameshawahi kuwa mabingwa wa 1975, 1994 na 2010 wamepangwa pamoja na ndugu zao, Zanzibar ‘Heroes’, Djibouti na mabingwa watetezi, Kenya ‘Harambee Stars’.


Kundi A linaundwa na wenyeji, Uganda, Burundi, Ethiopia na Eritrea, wakati Kundi B linaundwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan, Sudan Kusini na Somalia

Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitaingia Robo Fainali zikiungana na mbili nyingine zitakazomaliza na wastani mzuri katika nafasi ya tatu. 

CECAFA Challenge ndiyo michuano mikongwe zaidi ya soka barani Afrika ambayo ilianza mwaka 1926 ikijulikana kama Kombe la Gossage hadi mwaka 1966, ilipobadilishwa na kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati hadi mwaka 1971 ilipobadilishwa tena na kuwa CECAFA Challenge.


Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara saba, Ethiopia mara nne na Tanzania mara tatu.


Mara ya mwisho Tanzania Bara ilitwaa Kombe hilo mwaka 2010 mjini Dar es Salaam ikiwa chini ya kocha Mdenmark, Jan Borge Poulsen.

Post a Comment

0 Comments