BETI NASI UTAJIRIKE

HII HAPA MIPANGO YA AJIBU NDANI YA SIMBA

Kiungo mahili wa klabu ya Simba ameahidi kuifanyia mambo makubwa klabu hiyo iliyomsajili akitokea Yanga.Awali Ajibu aliichezea Simba na baadaye aliuzwa kwenda Yanga


Msimu huu amerejea tena Simba.Katika msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania , Ajibu akiwa Yanga alifanikiwa kuweka rekodi ya kutoa pasi za mabao 17, jambo ambalo linaonekana ni gumu kwake kufanya msimu huu kwani mpaka sasa ametoa pasi tatu tu za mabao.

Ajibu anatamani kuifikia rekodi aliyoweka akiwa na Yanga, kikubwa kwake ni kupata dakika nyingi za kucheza kama alivyokuwa akipata msimu uliopita akiwa na Yanga.

“Hakuna mtu asiyependa kupata mafanikio, mafanikio yangu ni kuona nakuwa bora zaidi ya msimu uliopita hivyo natamani nifanye zaidi ya nilivyofanya msimu uliopita nikiwa na Yanga,kikubwa nikupata nafasi nyingi zaidi ya kucheza.

“Nafasi ninayocheza hapa Simba wapo wachezaji wengi sana wenye uwezo kwani mwalimu anaweza kumtumia yeyote atakayemtaka, hivyo ili nipate nafasi ya kucheza kunahitaji bidii kubwa ya kumshawishi mwalimu kwa ajili ya kupata nafasi mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu uliopita nikiwa Yanga ambapo nilicheza mechi nyingi,” alisema mchezaji huyo.

Post a Comment

0 Comments